YANGA YATWAA UBINGWA BAADA YA AZAM KUTOKA SARE 1-1 NA COASTAL UNION
Kikosi cha Yanga
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salam
Klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo
imejitangaziwa ubingwa wake wa 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara baada
ya wapinzani wake wakubwa kwa muda mrefu klabu YA Azam fc kutoa sare ya
kufunga bao 1-1 na Wagosi wa kaya Coastal unioni katika dimba la CCM
Mkwakwani jijini Tanga.
Matokeo hayo yana maanisha, Azam FC
waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC waliojikusanyia pointi 56
kibindoni, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa
hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine mbili zilizobaki,
watamaliza na pointi 54.
Shukurani kubwa kwa nyota wa Coastal
union Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika
ya 72 akipokea pande maridhawa kutoka kwa nyota wa zamani wa Yanga Pius
Kisambale.
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata
bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti
dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence
Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari na beki Yussuf Chuma- na
refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.
Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal
kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu
waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani hao.
Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kulinda
heshima kutokana na kubakiwa na mechi mbili ambapo watashuka dimbani
kuvaana na Coastal union waliowapa ubingwa msimu huu pamoja na mechi ya
kufunga dimba dhidi ya Mnyama Simba uwanja wa Taifa Dar es salaam
Lakini licha ya Coastal union kuwapa
ubingwa wanajangwani hao, Kocha mkuu wa wagosi Wakaya Hemed Morroco
amesema mchezo wa leo walistahili kushinda na kilichokwamisha ushindi
leo ni waamuzi kuchezesha hovyo.
“Unajua Azam walikuwa na Presha kubwa
ya kutaka ushindi, lakini tuliwabana na waamuzi wameshindwa kuchezesha
vizuri na ndio maana wameambulia sare vinginevyo walikuwa wanafungwa
leo”. Alisema Morroco.
Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa;
Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma,
Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud
dk85, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Danny Lyanga dk71 na Twaha Shekuwe.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’.
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’.
No comments:
Post a Comment