IBF YATEUA REFARII NA MAJAJI PAMBANO KATI YA CHEKA NA MASHALI
NA: ONESMO NGOWI
Shirikishoi
la Ngumi la Kimataifa (IBF) limeteua refarii na majaji wa pambano la
kutetea ubingwa wa Afrika kati ya anayeushukilia ubingwa huo Francis
Cheka wa Tanzania na mpinzani wake Thomas Mashali ambaye ni bingwa wa
uzito wa Middle ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) Refarii
wa mpambano huo wa kukata na
shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka nchini Zambia mbaye alilisimamia
pambano kati ya Francis Chaka na Mada Maugo mwaka jana kwa ustadi
mkubwa. Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa
Zambia na ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
Aidha,
majaji wa mpambano huo ni Daudi Chikwanje kutoka Malawi ambaye ndiye
Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba
moja. Steve Okumu wa Kenya ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail
Sekisambu wa Uganda ambaye anakuwa jaji namba tatu. Msimamizi mkuu wa
mpambano huo ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.
Hata
hivyo Ngowi amemwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango na Ushindi wa
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) Boniface Wambura amshikie
nafasi hiyo ili Ngowi apate nafasi nzuri ya kusimamia mapambano matatu (
moja la ubingwa wa dunia kwa vijana,, lingine la ubingwa wa mabara kwa
wanawake na lingine ubingwa wa Afrika) yatakayofanyika nchini Ghana
tarehe 3 mwezi Mei.
Nayo
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini TPBC imeshateua maofisa
watakaosimamia mapambano ya awali pamoja na kutoa kibali kwa kampuni ya
Mumask Investment and Gebby ili iendeshe mpambano huo!
Hii
ni mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu
amsambaratishe kwa TKO bondia machachari Mada Maugo katika mpambano
uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili katika ukumbi wa PTA jijini Dar
Es Salaam.
No comments:
Post a Comment