MWANAFUNZI WA DSJ AFA, 22 WAJERUHIWA CHALINZE
Na Nyendo Mohamed.
WANAFUNZI wa Chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) wapata ajali katika eneo la Chalinze walipokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam ambapo wanafunzi ishirini na mbili wamejeruhiwa na mmoja kupoteza maisha pamoja na dereva aliyekuwa amewabeba wanafunzi hao.
Akizumgumza na wanahabari jana kiongozi wa msafara huo Victor Sinka alisema kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya jumapili juzi majira ya saa tatu na nusu usiku katika eneo la Chalinze walipokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar ea Salaam.
Alisema kuwa wanafunzi hao walikuwepo Mkoani Mbeya kwa takribani siku nne ambapo walikuwa katika ziara ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani humo na kutembelea baadhi ya vituo vya habari ambapo ziara hiyo atahusisha matokeo ya mtiahani wa mwisho wa wanafunzi hao.
Ziara hiyo ambayo ilkuwa idadi ya wanafunzi 180 wakiwemo wanafunzi wa ngazi ya Stashahada na cheti pamija na walimu 3 na msafara huo ulikuwa na jumla ya magari 6 aina ya costa.
Ambapo alisema chanzo cha ajili hiyo imesababishwa na lori lililokuwa limebeba mafuta baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo kuacha njia na kusababisha lori hilo kugongana na costa hiyo iliyobeba wanafunzi uso kwa uso na kusababisha dereva aliyekuwa akiendesha costa hiyo na wmwanafunzi mmoja kupoteza maisha na dereva wa lori akiwa amejeruhiwa na babadhi ya wanafunzi kujeruhiwa.
Aliongeza kwa kusema kuwa baada ya ajali kutokea majaruhi wote walipelekwa katika hospitali ya Tumbi ambapo Dereva aliyekuwa amebeba wanafunzi aliyefahamika kwa jina la Ally Zungu na mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Diedon Eliason Kibona wote walipoteza maisha ambapo waanfunzi wawili akiwemo Zubeda kishangi na Dorotea Sarara wakiwa wamejeruhiwa vibaya wote wakiwa katika ngazi ya shahada.
Afisa wa Habari wa serikali ya wanafunzi Alex Mallya amesema kuwa mawanafunzi huyo alikuwa akitumikia serikali ya wanafunzi wa Dsj akiwa kama Waziri Mkuu na kusema kuwa wamepokea msiba huo wa mwanafunzi mwenzao mpaka utakaposafirishwa kuelekea Tabora kwa wazazi wake kwa mazishi ambapo kwa sasa mwili wa marehemu huyo uliwa kwa mama mdogo wa marehemu Tabata Dar es Salaam.
Mallya alisema kuwa majeruhi wawili waliokuwa katika hali mbaya wameamishwa katika hospitali hiho ya Tumbi wameweza kutolewa kutokana na ndugu wa majeruhi hawa kuwaleta Dar es Salaam.
Aidha mmoja kati ya wwanafunzi aliyeshuhudia ajali hiyo Groly Amphrey alisema kuwa alishuhudia ajali hiyo baada ya kuona lori hilo likiwa linayumbayumba na ghafla aliona likiacha njia na kuvaana na gali walikuwa wamepanda na wanafunzi waliokuwa upande wa dereva kujeruhiwa vibaya.
Pia alisema kuwa baada ya kupata ajali wamepoteza baadhi ya vitu mbalimbali ikiwemo kamera, simu pamoja na mabegi yao na vibaka waliokuwa eneo hilo babada kutopata msaada wa haraka kutoka kwa polisi.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa Kamanda wa Pwani kuhusiana na ajali hiyo ameshindwa kupatikana kutokana na kupigiwa simu kwa muda mrefu na kutopatiakana.
No comments:
Post a Comment