TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, April 20, 2013

"ADHABU YA SIKU TANO KWA WABUNGE WA CHADEMA HAITOSHI...WAFUKUZWE MIEZI MITATU".....HII NI KAULI YA MHADHIRI WA UDSM

 Kitendo  cha  wabunge  sita  wa  CHADEMA  kufukuzwa  juzi  bungeni  limezidi  kuchukua sura  mpya  hapa  nchini....

Wapo  wanaodai  kuwa  adhabu  hiyo  haikuzingatia  kanuni  za  bunge  na  badala  yake  ilitolewa  kwa  jazba  za  Naibu  spika  wa  bunge.....

Mbali  na  hao, lipo  kundi  linaloamini  kuwa  adhabu  hiyo  ni  sahihi  na  wanadai  kuwa  ni  ndogo  na  pengine  ingekuwa  vyema  kama  ingeongezwa  ili  liwe  fundisho  kwa  wabunge  wengine

Kwenye kipindi cha tuongee asubuhi Star TV ,mhadhiri mwandamizi wa  chuo  kikuu  cha  Dar es Salaam ( UDSM), Dr Bana, amesikika  akisema  kuwa   adhabu waliopewa akina Lissu ya siku tano haitoshi na walitakiwa wapewe adhabu hata ya miezi mitatu na wakatwe mishahara pia.

Kauli  hiyo  imeibua  maswali  mengi  miongoni  mwa  wachambuzi  wa  mambo  ya  kisiasa  wanaodai  kuwa   iwaje  mbunge  afukuzwe  kwa  kuomba  MWONGOZO  wakati  aliyetukana  tusi  la  nguoni  "Come-on Fu*ky  you"  ameachwa???

No comments:

Post a Comment