PINDA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU
Askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa mtu aliyepoteza maisha kutokana na
kuporomoka kwa udongo katika machimbo ya Moramu yaliyopo eneo la
Moshono, Arusha.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana
alitangaza kuyafunga rasmi machimbo ya moramu eneo la Moshono, Arusha
hadi Serikali itakapoweka utaratibu mzuri wa shughuli mbalimbali za
uchimbaji katika eneo hilo.
CHANZO:MWANANHI.
Hatua hiyo ya Pinda imetokana na
ajali ya watu 14 waliopoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi juzi,
wakati wengine wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo iliyochangiwa kwa
kiasi kikubwa na mvua zinazonyesha jijini Arusha.
Pinda alitoa agizo hilo alipotembelea
eneo hilo pamoja na kuwajulia hali majeruhi wawili waliolazwa katika
Hospitali ya Mkoa ya Mt MeruCHANZO:MWANANHI.
No comments:
Post a Comment