TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, July 8, 2013

THIAGO,VILLA KUMNG'OA ROONEY MAU UNITED
rooney ab6ca
 Mshambuliaji wa Man U, Wayne Rooney (HM)

thiago d182e
 Thiago Alcantara
 villa 9280b
David Villa
KLABU ya Barcelona inataka kuwatoa Thiago Alcantara na David Villa sambamba na kiasi fulani cha fedha Old Trafford ili wapewe Wayne Rooney akacheze Hispania.
 Vigogo hao wa Katalunya wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji licha ya kwamba tayari wanaye Neymar waliyemsajili mwezi uliopita.

Rooney, ambaye aliishuhudia Fainali ya michuano ya Tenisi ya Wimbledon jana Andy Murray akitwaa taji upande wa wanaume, anakabiliwa na kiza juu ya mustakabali wake Manchester United na aliomba kuondoka mwishoni mwa msimu.
Arsenal na Chelsea bado wana matumaini ya kumnasa mshambuliaji huyo wa England ahamie London, ingawa ukweli unabaki hilo litakuwa jambo gumu kwa United kuwauzia silaha wapinzani.

Rooney na David Moyes wamekwishazungumza juu ya mustakabali wake: wawili hao walikutana nyumbani kwa Rooney kabla hata wachezaji hawajarejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wiki iliyopita, na Mscotland huyo akaweka wazi katika Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari wiki iliyopita.

Kocha huyo mpya wa United anatarajiwa kutoa taarifa yake ya usajili baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson rasmi mapema mwezi huu.
Na hiyo imelifanya gazeti la Sport la Hispania kuandika kwamba Rooney anaweza kutumika kuongeza ubora La Liga.

Taarifa katika gazeti hilo imesema kuondoka kwa Thiago kwa kiasi cha Pauni Milioni 17 ni kama kunawezekana na zaidi katika dili hilo, Villa pia, mwenye thamani ya Pauni milioni 8.5 ataondoka Nou Camp akiwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake.

Pamoja na hayo, Pauni Milioni 4 taslimu itaongezwa ili kufikisha tahamani ya Rooney, zaidi ya Pauni Milioni 30. Chanzo: Sportmail

No comments:

Post a Comment