TENGA: HAKUNA HILA KWENYE MAREKEBISHO YA KATIBA
Rais wa TFF, Leodgar Tenga
RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema
hakuna hila yoyote katika marekebisho ya Katiba kwa vile yametokana na
maagizo ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA). (HM)
Akizungumza na Wahariri wa Michezo
kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam jana (Julai 9 mwaka huu), Rais Tenga
amewahakikishia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Dharura kuwa dhamira ya
marekebisho hayo ni nzuri, kwani lengo ni kila mtu apate haki yake.
Amesema Mkutano huo utakaofanyika
Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) utakuwa na ajenda moja tu ya kuingiza
Kamati ya Maadili, na Kamati ya Rufani ya Maadili katika Katiba ya TFF
kama ilivyoelekezwa na FIFA ili baadaye uanze mchakato wa uchaguzi.
“Katika kuunda Kamati ya Maadili
tumeangalia ile ile ya FIFA, tusitengeneze kitu kipya, yaondolewe yale
yanayotakiwa kuondolewa, na yaongezwe yale yanayotakiwa kuongozwa. Kwa
sababu tumeangalia mazingira kwa Tanzania ni tofauti na Ujerumani au
nchi za sehemu zingine,” amesema.
Rais Tenga amewataka wajumbe wafike
kwenye Mkutano wakiwa na mtazamo wa kujenga, kwani kuna maagizo ya FIFA
ambayo wanatakiwa kuyatekeleza ili wasonge mbele.
“Tutawaeleza kwanini hili limewekwa na
lile limeondolewa. Mpira unataka unit (kitu kimoja), ni mchezo wa kila
mtu. Baada ya hapa tunaanzisha mchakato wa uchaguzi. Watu wanaingia
wakiwa wamoja, wanatoa hoja wanasikilizwa. Wanahukumiwa kwa hoja,”
amesema na kuongeza utatolewa muda wa kutosha wajumbe ili wayaone na
kuelewa marekebisho hayo.
Rais Tenga pia alizungumzia kipindi
hiki cha usajili na kutaka klabu ziwaachie wataalamu wa mpira wa miguu
kwani ndiyo wanaojua upungufu wa timu, hivyo wanaweza kusajili wachezaji
sahihi.
Amesema tatizo kubwa la klabu za
Tanzania ni kuwa timu zao hazina uwezo wa kuhimili dakika 90, hivyo watu
wanapaswa pia kuzungumzia aina ya mazoezi ambayo timu zao zinafanya
badala ya kubakia kutaja tu majina ya wachezaji wanaotaka kusajiliwa.
Chanzo: Boniface Wambura
No comments:
Post a Comment