TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, July 4, 2013

ROONEY ATAKIWA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KUONDOKA MAN U

runi 2ab1c
 Mshambualiaji Wayne Rooney (HM)

rooney daf64

moyes b825a
Kocha wa Man U, David Moyes jana alikutana na Rooney

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney atatakiwa kuwasilisha barua ya maandishi ya kuomba kuondoka ikiwa anataka kuachana na  Manchester United.

Mpachika mabao huyo wa Old Trafford, alirejea mazoezini jana huku mustakabali wake ukiwa bado haueleweki. Imefahamika hakuwa na Mkutano mahsusi na kocha mpya David Moyes juu ya suala lake. 

Hilo linaweza kutokea katika kituo cha mazoezi cha klabu, Carrington leo. Wawili hao walizungumza jana, lakini si kwa muda mrefu na msimamo wa United kwake bado haujabadilika.

Wamesema mshambuliaji huyo wa England hauzwi. Kuhusu tetesi za wapinzani wao katika Ligi Kuu, Arsenal kutaka rasmi kumsajili tangu wiki iliyopita, United bado haijawasiliana na yoyote anayemtaka Rooney.

Sakata hili linaweza kugeuka tu iwapo mshambuliaji mwenyewe ataamua kulazimisha kuondoka. BIN ZUBEIRY iliandika mwishoni mwa msimu uliopita kwamba, Rooney aliomba kuondoka kwa kocha aliyestaafu, Sir Alex Ferguson.
Ombi la kuondoka litamaanisha Rooney hatadai chochote katika Mkataba wake wa miaka miwili uliobakia ambao alikuwa analipwa pauni 250,000 kwa wiki. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment