TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, July 16, 2013

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA , BUXTON CHIPETA AFARIKI DUNIA



Jaji Buxton Chipeta.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania, Buxton Chipeta amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.

Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
 

Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
 

  Habari makini inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.

No comments:

Post a Comment