TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, July 11, 2013

CHELSEA YASAJILI KIPA MARK SCHWARZER
10 62623
Kipa Mark Schwarzer
20 c6f8e
Schwarzer akisaini mkataba
30 dee6f
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akisalimiana na Schwarzer
KIPA Mark Schwarzer amesani Mkataba wa mwaka mmoja Chelsea, baada ya kuondoka Fulham mwishoni mwa msimu kufuatia kumaliza  Mkataba wake.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 amechezea klabu za Bradford City, Middlesbrough na hivi karibuni Fulham, kwa kipindi cha miaka 17.
"Ni klabu babu kubwa,"alisema kuiambia tovuti ya Chelsea. "Ni moja ya klabu kubwa na bora duniani, na ni heshima kusaini Chelsea. Sikushawishiwa kwa kiasi kikubwa kuja hapa,"alisema.
Kipa huyo wa kimataifa wa Australia, ameisaidia nchi yake kufuzu Fainali za Kombe la Dunia Brazil mwakani, na pia atakuwa nyumba ya kipa namba moja Chelsea, Petr Cech, ingawa atapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika mashindano mbalimbali.
Ameidakia mechi 108 Australia, na mafanikio yake makubwa England ni pamoja na kutwaa Kombe la Ligi akiwa na Middlesbrough mwaka 2003 na kucheza Fainali za KOmbe la UEFA mwaka 2006 na Europa League mwaka 2010. Chanzo: Sportmail

No comments:

Post a Comment