WABUNGE WAANZA KUJIHAMI NA MILIPUKO YA MABOMU....WAMEOMBA ULINZI UIMARISHWE BUNGENI
MBUNGE wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.
Ndasa
aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu kurushwa katika
sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi
la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 50
kujeruhiwa vibaya.
“Mheshimiwa
Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana hofu ya
kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa hafifu,” alisema
Ndasa.
Ndasa
alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha hivyo
ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara makubwa kwa
taifa.
Wabunge
leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila
anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.
No comments:
Post a Comment