UPDATE: RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali
nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la
kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60
wamejeruhiwa.
Rais Kikwete alikuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amekatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait.
Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
No comments:
Post a Comment