RIPOTI MWANDISHI MMOJA HUUAWA KILA BAADA YA SIKU 5 DUNIANI
Askari Polisi wakiwa katika eneo
alipouawa Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi kwa kulipuliwa na bomu la
machozi mwaka jana. Picha na Maktaba
Dar es Salaam. Mwishoni
mwa wiki tasnia ya habari ilifanya kumbukumbu ya Siku ya Uhuru wa
Habari huku taarifa zikionyesha kuwa kwa miaka kumi iliyopita, wastani
wa mwandishi mmoja kuuawa kila baada ya siku tano katika maeneo
mbalimbali duniani.
Ripoti iliyoandaliwa na jumuiya ya
kulinda usalama wa waandishi wa habari duniani (CPJ) inaeleza kuwa
tangu mwaka 1992 mpaka 2013, waandishi 982 wameuawa.
Sababu za mauaji hayo zinatajwa kuwa ni mazingira ya utekelezaji wa kazi zao.
Ripoti ya CPJ inaonyesha nchi za
Afrika na Uarabuni zinaongoza katika utekelezaji wa mauaji hayo huku
Somalia ikiripotiwa kuuawa waandishi 50 katika kipindi hicho.
Nchi kubwa zenye idadi ndogo ya mauaji hayo ni Uingereza(1), Ufaransa(1), China (2), Japan (1)na Hispania(1). Tanzania ni moja kati ya nchi zilizotajwa na kuingia katika ripoti ya kumbukumbu hiyo duniani kutokana na kifo cha mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

Pia, mwanahabari Issa Ngumba wa Radio Kwizera aliuawa kule Kakonko, Mkoani Kigoma.
Kutokana na matokeo hayo, wadau
mbalimbali wa masuala ya habari nchini wametoa maoni yao juu ya
mwenendo wa uhuru wa vyombo vya habari nchini wakisema uhuru huo sasa
umetiwa kitanzini.
MCT
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga amesema katika kipindi cha hivi karibuni usalama kwa waandishi wa habari umepungua kutokana na kuwapo kwa matukio ya vitisho visivyotarajiwa miongoni mwao.

Mukajanga alisema mbali na mauaji ya Mwangosi, kuna baadhi ya vitisho vimetolewa kwao wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Matukio ya utekaji nyara japokuwa
hatujapata uthibitisho lakini hali hiyo imeondoa taswira ya nchi na
kushusha heshima yake kimataifa,” alisema Mukajanga.
Mukajanga alisema matukio hayo
yamesababishwa na hali ya kuibuka kwa makundi ya kisiasa na kidini
katika kipindi cha hivi karibuni hatua iliyochangia mwandishi kunyimwa
uhuru na kujengewa dhana ya kuegemea upande mmoja katika uandishi wa
habari zake hususan zinazogusa makundi hayo.
“Kwa mazingira hayo mwandishi wa
habari lazima atakuwa na wakati mgumu sana, hata kama ataandika ukweli
bado atakuwa amesababisha madhara au kuharibu masilahi ya upande
mwingine,” anasema Mukajanga.
Hata hivyo, Mukajanga alitoa
mapendekezo yake akiwataka waandishi wan habari kusimamia maadili ya
kazi zao ili jamii itambue ukweli hata kama wataendelea kupigwa vita.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Erenest Sungura alisema kutokana na usalama wa mwandishi wa habari kupungua hapa nchini, Serikali inatakiwa kuangalia changamoto za kimazingira zinazochangia madhara hayo.
Sungura alisema inawezekana moja ya
sababu ni pamoja na sheria zinazonyima uhuru wa kuandika habari fulani
hivyo mwandishi hujikuta akilazimisha kuandika ukweli katikati ya
ukiukwaji wa sheria zinazombana.
“Kuna sheria zinazowanyima uhuru wa kuandika mambo mengine zifanyiwe mabadiliko,” alisema.
Hata hivyo, Sungura anatoa wito
akiwataka wamiliki wa vyombo vya habari kutengeneza mazingira ya ulinzi
wa kutosha kwa waandishi wao pale wanapokuwa wanafanya kazi za
uchunguzi.
“Wahariri waangalie suala hilo kwa
sababu mimi napokea simu karibu tano kwa mwezi za waandishi wakieleza
kupewa vitisho,” anasema.
Mbali na hilo, Sungura anawataka pia waandishi wazingatie maadili ya kazi zao ili kujenga taswira ya ubora wa taaluma yao ili kujiweka huru na kupunguza uadui miongoni mwa jamii zenye makundi.
Mbali na hilo, Sungura anawataka pia waandishi wazingatie maadili ya kazi zao ili kujenga taswira ya ubora wa taaluma yao ili kujiweka huru na kupunguza uadui miongoni mwa jamii zenye makundi.
Taswa
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa), Juma Pinto anasema tofauti za makundi ya kisiasa ndiyo imekuwa chanzo cha mwandishi wa habari nchini kukumbwa na hatari ya usalama wake pale anapokuwa akitekeleza majukumu yake.

“Makundi ya kisiasa ndiyo tatizo zaidi, kwa nini hatusikii kwenye michezo au burudani,” alisema.
Pinto anasema kutokana na mazingira
magumu yaliyopo kwa sasa, ameshauri waandishi kuwa na umoja na msimamo
mkali pale inapotokea mwandishi ameingia kwenye matatizo ya vitisho,
kutekwa au kuuawa.
“Mbali na msimamo wetu Serikali pia
inatakiwa kuangalia sheria kandamizi kwa mwandishi wa habari, Katiba
yenyewe inamtambua mmiliki wa chombo na sio mwandishi, yaani mwandishi
wetu hapa nchini ni sawa na mtoto aliyetelekezwa, hana sehemu yoyote
inayomtambua,” anasema Pinto.
Hali katika nchi nyingine
Mbali na taarifa hizo, hali si salama kwa nchi nyingine ambapo shirika la waandishi wa habari wasio na mipaka duniani liliripoti kuwa mwaka 2012 ulikuwa ni mwaka wa maafa zaidi kwa waandishi wa habari kote duniani ukilinganisha na miaka iliyopita.

Somalia ambayo haina serikali thabiti iliripotiwa kufanya mauaji ya waandishi 18 na Pakstan waandishi 10.
Katika ripoti hiyo ya Desemba 19,
2012, ofisa wa shirika hilo, Ulrike Gruska anasema waandishi 88
waliuawa wakati wakiripoti kazi zao kutoka maeneo yenye vita na
mashambulizi ya mabomu huku sababu zikielezwa kuwa ni pamoja na
mazingira ya kutatanisha, makusudi na uhasama kutoka kwa baadhi ya
wanasiasa.
Ripoti hiyo inasema mpaka sasa kuna
jumla ya waandishi wa habari 65 wameuawa nchini Syria mwaka huu, wakati
wanatekeleza majukumu yao, huku 21 wakiswekwa rumande na makundi ya watu
ama wapiganaji nchini humo.
Nchini Mexico, waandishi wanaishi
katika maisha ya hatari,hasa wanapokuwa wanaripoti kuhusu uhalifu,
usafirishaji wa dawa za kulevya na uhusiano kati ya viongozi wa magenge
ya wahalifu na wafanyakazi wa umma.
Taarifa nchini humo zinasema kuna idadi ya waandishi sita wameuawa tangu Januari mwaka huu.
Mbali na nchi hiyo, Brazil pia
imetajwa kama mojawapo ya nchi hatari kwa waandishi wa habari kutokana
na vita inayofanywa dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Matukio ya unyanyasaji
Katika hatua nyingine, hali imeonyesha wasiwasi baada ya kuongezeka kwa idadi ya waandishi duniani waliofungwa jela mwaka huu. Ripoti hiyo inasema zaidi ya waandishi na wana ‘blogi’ 1,000 walikamatwa mwaka huu huku zaidi ya 2,000 wakipewa vitisho. Chanzo: www.mwananchi.co.tz

No comments:
Post a Comment