DOTNATA AWEKEWA TEGO LA SUMU KWENYE JUICE
Muigizaji wa filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu
kwenye juice na mtu asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa
ya kiafya.
Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa kwenye
hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku wakimweleza
huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa uchunguzi wa moyo
kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa vipimo zaidi.
Anasema tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi alikuwa akitapika.
“Nimezidiwa usiku wa kuamkia Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa
ikabidi wanichunguze kwa makini kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua
nimelishwa sumu takriban mwezi wa nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu
aliipitisha kwa njia ya juice,” amesema Dotnata ambaye kwa sasa
ameokoka.
Akizungumzia sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
“Kila mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda
hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua
mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili
niyasimulie mema ya Mungu.
Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako
kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”
No comments:
Post a Comment