TAFF YATOA ONYO KWA WASANII
SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limekemea baadhi ya
wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko
‘Sajuki’.
Pia limesisitiza kuwa msanii atakaeripotiwa katika vyombo
vya habari kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa TAFF,
Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha wasanii kuacha msiba na
kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa dini.
Alisema baadhi ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu
katika msiba wa marehemu Kanumba na wengine katika msiba wa Sajuki.
“Nasikitika kuona msanii hajitambui hata kidogo, yani
anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na mahala pa msiba, jamani huu
msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya katika misiba TAFF tutamfungia”
alisema Mwakifwamba.
Katika hatua nyingine alisema msiba huo ulitawaliwa na
utani hali ya kwamba umewakutanisha watani wa makabila.
No comments:
Post a Comment