MENEJA WA MACHINGA COMPEX DAR AVINJWA MKONO
MGOGORO wa vizimba katika soko la wafanyabiashara wadogo la Machinga Complex lililoko jijini Dar es Salaam umeingia hatua nyingine baada ya Meneja wa soko hilo, Nyamsukura Masondore kuvamiwa na wafanyabishara hao, kumpiga hadi kumvunja mkono.
Tukio
hilo lilitokea Januari 7, mwaka huu, wakati Meneja huyo akiwa ziarani
kuhakiki umiliki halisi wa mpangaji na ulipaji wa kodi kwa vizimba
hivyo.
Akiwa
katika mahojiano na Mwananchi, Msondore alisema kuwa wakati wa zoezi
hilo la kuhakiki wapangaji na walipakodi ghafla alivamiwa na watu
wasiopungua wanane na kumpiga hadi kumvunja mkono.
“Nilikuwa
nimeongozana na viongozi wenzangu kwenye shughuli hiyo ya uhakiki,
ghafla nikavamiwa na watu ambao wanadaiwa ni wafanyabiashara wa hapa
kwenye jengo na wengine wa Soko la Karume wakanipiga hadi kunivunja
mkono,” alisema Masondore.
Masondore
alisema kuwa alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Pangani katika
Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam na kupewa RB ya polisi no
Ila/rb/75/2013 kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili, na uchunguzi wa
polisi unaendelea.
Aliongeza
kuwa kutokana na tukio hilo alishindwa kuendelea na uhakiki huo wa
vizimba na walipakodi na kuelekea Hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya
Ilala jijini Dar es Salaam ambapo ndipo anapata matibabu hadi sasa.
MWANANCHI
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi Komba alisema kuwa
hana taarifa za kutokea kwa vurugu hizo katika jengo hilo la
wafanyabiashara wadogo.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa jengo hilo, Abubakari
Rakesh ameulalamikia uongozi wa jengo kuwa tangu kuzinduliwa kwa gulio
lililopo ndani ya jengo hakuna ufuatiliaji wowote uliofanyika ili
kuutaka kujua maendeleo ya wafanyabiashara.
Alisema
kuwa uzinduzi huo ambao ulifanywa na Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dar
es Salaam, Abdalah Chaurembo haukuwa wazi kwa kila mtu jambo ambalo
halikupangwa kufanyika hivyo tangu taratibu hizo za uzinduzi zianze.
“
Uzinduzi huu ulikuwa wa kimyakimya jambo ambalo hatukupanga hivyo,
tulitegemea matangazo mbalimbali yawekwe kwa ajili ya kuwakumbusha
wafanyabiashara na wananchi pia juu ya uzinduzi, lakini haukufanyika
hivyo, naweza kusema ulikuwa uzinduzi wa funika kombe mwanaharamu
apite”, alisema Rakeshi.
Rakesh
aliongeza kuwa uongozi wa jengo hilo ulitakiwa uwe mstari wa mbele kwa
ajili ya kutetea maslahi ya wafanyabiashara wanaofanya biashara zao hapo
lakini badala yake uongozi huo haupo bega kwa bega na wafanyabiashara
hao.
No comments:
Post a Comment