IFM YAISIFU TANZANIA KWA KUDHIBITI MFUMUKO WA BEI
Na: Heka Paul- Maelezo
Shirika
la Fedha Duniani(IMF) limepomngeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa
kisera ambao umesaidia utulivu wa kiuchumi ambao umesaidia kuleta
matumaini hatua iliyosababisha mfumuko wa uchumi hapa nchini kuendelea
kushuka.
Kauli
hiyo Mwakilishi Mkazi nchini wa IMF Thomas Baunsgaard wakati wa mkutano
wake yeye na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na waandishi wa habari
jijini Dar es salam juu ya kuelezea tathmini ya mapitio ya mwenendo wa
uchumi wa Tanzania iliyofanywa na Shirika la fedha duniani(IMF) .
Alisema
kuwa ni muhumu wa kuendelea kudhibiti sera za mapato na matumizi ya
serikali na sera za usimamizi wa fedha ili kuwa na uchumi endelevu.
Bw.
Baunsgaard alisema kuwa Tanzania imedhamiria kuchukua hatua za ziada
ili kuhakikisha inafikiwa lengo la kupunguza mfumuko wa bei hapa nchini.
Aidha
alisema kuwa Bodi ya utendaji wa shirika la IMF imeidhinisha nyongeza
ya dola za Kimarekani 57 na kuifanya Tanzania kuweza kunufaika na mkopo
wenye masharti nafuu toka IMF unaofikia dola zaa kimarekani 114.
Vilevile
Bodi iliridhia ombi la Serikali ya Tanzania la kupewa msamaha wa
kukuika kigezo cha madeni ya nje yenye masharti ya kibiashara kwa sababu
ukiukaji huo hauwezi kuathiri uhimilivu wa deni la Taifa.
No comments:
Post a Comment