WAZIRI ACHARUKA UCHAFU WA SOKO LA FERI
WAZIRI wa
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo, ametishia
kuinyaing’anya Halmashauri ya Manispaa Ilala usimamizi wa Soko la Samaki
Feri endapo itaendelea kuliacha soko hilo katika hali ya uchafu.
Akizungumza na Fullshangweblog jijini
Dar es Salaam jana, Dk. Mathayo alisema wizara yake haiko tayari kuona
hali ya uchafu ikiendelea bila ya kupatiwa ufumbuzi.
“Tumekuwa tukiwasisitiza wafanye usafi
ili Watanzania waweze kula chakula chenye ubora kwa ajili ya afya zao,”
alisema Dk Mathayo.
Alisema halmashauri hiyo bado ina
nafasi ya kutafuta mbinu mbadala za kulifanya soko hilo katika hali ya
usafi, ili kuepuka hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa na na wizara hiyo.
Hata hivyo, alisema kabla ya kufikia
hatua hiyo, wizara itabidi ikutane na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Unajua hiki ni kitu cha watu wengi ni
lazima kila mtu ahusishwe katika maamuzi yanayoweza kufikiwa na kwa
ajili ya maslahi ya wananchi ambao ndiyo wadau wa soko hilo, ” alisema
Dk. Mathayo.
Awali, baadhi ya wananchi walieleza
kushangazwa kutotekelezwa kwa ahadi iliyotolewa na wizara hiyo kwa zaidi
ya miezi sita sasa kuwa endapo halmashauri hiyo itashindwa kudhibiti
uchafu, italinyanganya usimamizi.
Kutoka fullshangweblog
No comments:
Post a Comment