TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, January 30, 2013

MANJI ALIA NA UGUMU WA KUENDESHA TIMU
Na Khadija Mngwai
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji (pichani), ameibuka na kusema anakumbana na ugumu mkubwa katika kuiendesha klabu hiyo tangu alipopata nafasi ya kuwa mwenyekiti, Julai mwaka jana.
 Manji amesema anakutana na changamoto nyingi likiwemo suala la ukata.
Manji ambaye anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Bara katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24, mwaka huu, amesema klabu hiyo ina mambo mengi ya kimaendeleo inayotakiwa kufanya lakini tatizo kubwa ni ukata.
“Kwa kweli nimeona matatizo mengi yanayozikabili klabu zetu hapa nchini, hasa suala la ukata, kwani tangu nimeingia kuwa mwenyekiti ndiyo nimeona hali jinsi ilivyo na kuona ugumu unaozipata klabu zetu hapa nchini, awali nilikuwa sijui suala hilo.
“Klabu zinakumbana na ukata mkali, hasa zikiwa zinajiandaa na ligi, ndiyo maana nimeamua kuwania nafasi hii ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, kwani klabu hazina fedha, hali inakuwa ngumu na kusababisha timu kutokuwa na viwango,” alisema Manji.

No comments:

Post a Comment