SAKATA LA GESI MTWARA MBATIA NA WABUNGE WAKE HATIANI
Na: Nuzulack Dausen na Abdallah Bakari, Mtwara
MWENYEKITI
wa NCCR Mageuzi, James Mbatia jana alijikuta katika wakati mgumu baada
ya kulazimika kufungiwa katika ofisi ya NCCR-Mageuzi wilaya ya Mtwara
Mjini kutokana na baadhi wa wananchi walioudhuria mkutano wake wa
hadhara uliofanyika uwanja wa Mashujaa, kutaka kumdhuru kwa madai kwamba
hawakuridhishwa na hotuba yake.
Mbatia
alianza kurushiwa chupa tupu za maji alipokuwa akitoka uwanjani hapo
baada ya kukatisha hotuba yake kutokana na baadhi ya wananchi kupinga
kauli zake kwa madai hawamuelewi.
Kauli
inayodaiwa kumgharimu Mbatia ni ile ya ‘Iwapo gesi itatoka Mtwara’
ndipo wananchi hao walipoanza kupaza sauti wakisema
“Hatukuelewi…hatukuelewi” hata hivyo Mbatia aliendelea kuhutubia hali
iliyosababisha wananchi hao wapaze sauti zao kwa kuimba nyimbo.
“Haitoki…
Hatoki…Haitoki…” sauti za wananchi zilisikika na hata Mbatia
alipojaribu kuwatuliza wananchi hao kwa kusema ‘gesi kwanza…. Gesi
kwanza” baadhi waliitikia na wengine waliendelea kusema hawamuelewi.
Hali
hiyo ilimlazimisha Mbatia kukatisha hotuba yake saa 11.25 jioni na
aliondoka uwanjani hapo kwa kutembea kwa miguu hali iliyotoa mwanya kwa
wananchi kumrushia chupa tupu za maji. Mwenyekiti huyo akiwa ameambatana
na wabunge wa chama hicho, Moses Machali (Kasulu Mjini) na Agripina
Buyogela (Kasulu Vijijini) mkoani Kigoma, walielekea kituo cha polisi
kilichopi karibu na uwanja huo na baadaye alielekea ofisi za NCCR
Mageuzi wilaya.
Alipotafutwa
jana kuzungumzia suala hilo, Mbatia hakupatikana kupitia simu zake zote
za mkononi hata wabunge Buyogela na Machali pia simu zao zilikuwa
zimefungwa.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mtwara, Mary Nzuki alisema hakuwa na taarifa za
Mbatia kunusurika kupigwa ila aliahidi kufuatilia suala hilo.
“Ninachojua Mbatia yuko hapa kweli na amefanya mkutano wake, baada ya
mkutano ule akiwa anatoka eneo la mkutano alikuwa anasindikizwa na
wafuasi wake ambao walikuwa wanamshangilia. Sasa kama walipofika huko
mbele walimgeuka hilo sijui”, alisema Nzuki.
Pinda afunguka
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewasihi wakazi wa mikoa ya Kusini
kuwa wavumilivu na kuruhusu mradi wa kusafirisha gesi kutoka mikoa hiyo
kwenda Dar es Salaam ufanikiwe kwa kuwa una faida kubwa kwao.
Pinda
alitaja manufaa hayo kuwa ni pamoja na ajira kwa vijana watakaoshiriki
katika ujenzi huo, ujenzi wa viwanda na miundombinu na upanuzi wa
Bandari ya Mtwara.
“Nilishangaa
kuona wananchi wa Mtwara wanaandamana kupinga ujenzi wa bomba la gesi
asilia kutoka huko kwenda Dar es Salaam. Mradi huo ndiyo utakuwa
suluhisho la tatizo la umeme nchini, ”alisema Pinda na kuongeza:
“Wananchi
wa Mtwara wawe wavumilivu, watanufaika sana na mradi huo. Mradi
utajumuisha upanuzi wa Bandari ya Mtwara pamoja na ujenzi wa Viwanda
mbalimbali vitakavyosaidia kukuza uchumi wa maeneo yao kwa kutoa ajira
na kukuza biashara zao.”
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment