WAZIRI MKUU KUHAMASHISHA UCHANGIAJI WA VIKOBA VYA WATU WENYE ULEMAVU
Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiasalimiana Regina Mengi mtoto wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP . |
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema suala la uchangiaji wa
VICOBA kwa ajili ya watu wenye ulemavu linahitaji kupangiwa mkakati
maalum ili zipatikane fedha za kutosha kuwapa mitaji nao pia
wajitegemee.Amesema yuko tayari kukaa na Mkurugenzi Mtendaji wa
IPP, Bw. Reginald Mengi ili wabungue bongo ya jinsi ya kutunisha mfuko
wa VICOBA kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ametoa ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Januari 20, 2013)
wakati akizungumza na watu wenye ulemavu wa mkoa wa Dar es Salaam katika
hafla yao ya chakula cha mchana ya kuukaribisha mwaka mpya 2013
iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo iliandaliwa na Bw. Mengi.
“Bwana Mengi amewasha moto mzuri kwa kuwachangia hawa watu
sh. milioni 100. Nimeambiwa kuwa walianza kwa kujichangisha sh. milioni
17. Najua nami nawajibika kuwachangia lakini itabidi nikae naye tuone
jinsi huduma hii inavyoweza kusambaa na kuwafikia Watanzania wengi
zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Alisema ili uwe mpango endelevu, wabuni mpango
utakaowajumuisha Watanzania wengi zaidi, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa
dini na wengine wengi. “Nia yetu ni kila mwenye nacho achangie ili
kuwasadia wenzetu wawe na miradi ya kujikimu kimaisha kupitia mikopo ya
VICOBA,” alisema.
No comments:
Post a Comment