TAMKO LA MBATIA KUHUSU KUFANYIWA VURUGU MTWARA
Mwenyekiti wa chama cha NCCR
Mageuzi James Mbatia amedai kufanyiwa vururugu katika ziara yake Mtwara
na watu wanaodaiwa kutumiwa na baadhi ya wanasiasa.
Mbatia
amesema hao watu walianza hizo vurugu kwa kile kinachodaiwa kuwa
hawakufurahishwa na kauli yake ya kuwataka kukubaliana na serikali
kutaka gesi ambayo imegunduliwa itoke nje ya Mtwara.
Mbatia amesema asilimia 90 au 99 ya wananchi walikubaliana na kauli ya kutumia gesi kwa pamoja.
“Tukaelezana vizuri kwamba gesi
itakayotoka baharini ambayop ni takribani asilimia 78 ya gesi yote
ambayo imeshagundulika mpaka sasa, kituo cha kuisafisha kitakua palepale
Mtwara na ikishasafishwa, inasafirishwa na kuuzwa na wanamtwara
wanapata mrabaha kwenye hiyo itakayokua inasafirishwa, kimsingi hayo
tuliyazungumza na mkutano ulikwenda vizuri, jazba zilishuka na naweza
kusema zaidi ya asilimia ya 98 au 99 ya mkutano ule walikua vizuri” –
James Mbatia
“Waliofanya fujo ni kikundi cha
vijana ambao walikua wameandaliwa na chama cha siasa kwa ajili ya
kufanya fujo kwenye mkutano huo, walikua kama 30 mpaka 40 wakawa
wanataka maneno maneno lakini sisi tukafanya mkutano wetu vizuri,
tukamaliza nikatembea manake ni karibu na ofisi yetu ambapo pia hao
vijana walitufata kama kuja kufanya fujo lakini baadae jeshi la polisi
likaingilia kati na kuwachukua wachache” – James Mbatia
No comments:
Post a Comment