TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, January 30, 2013

LULU: SITAKI SHEREHE YA KUPONGEZWA BAADYA YA  KUTOKA MAHABUSU
Elizabeth Maiko "Lulu"

Marehemu Steven Kanumba

Na Mwandishi Wetu

STAA wa muvi aliyeachiwa huru kwa dhamana kufuatia madai ya kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mcheza filamu mahiri wa Bongo, Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anasemekana amegomea sherehe za kumpongeza kwa kutoka mahabusu, Risasi Mchanganyiko limekusanya data.
Lulu aliachiwa huru kwa dhamana juzi Jumatatu baada ya kusota kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa miezi 10 kwa kesi hiyo  ambayo imekuwa gumzo.
Kwa mujibu wa habari za kindugu, Lulu aligomea sherehe hiyo baada ya kusikia minong’ono ya kuwepo kwake kutoka kwa baadhi ya ndugu kwamba, akitoka watamuangushia bonge la pati.
Akijibu swali la paparazi wetu kuhusu sherehe hiyo, ndugu mmoja wa staa huyo (jina lipo) ambaye alikuwepo mahakamani hapo, alimkariri Lulu kwa kusema:
“Alisema sitaki sherehe kwa vile bado nina kazi kubwa mbele yangu, namwomba Mungu anisaidie katika safari ndefu ya kesi hii.”
Baada ya kumalizana na ndugu huyo, paparazi wetu alimfuata mama wa Lulu, Lucresia Karugila ambaye alikuwa katika hekaheka za kukamilisha taratibu za dhamana na kumuuliza kuhusu kuwepo kwa sherehe hiyo.
Hata hivyo, mama huyo alijibu kwa mkato: “Sina cha kuongea na nyinyi kwa sasa.”
KUTEMBELEA KABURI LA MAREHEMU KANUMBA
Wakati huohuo, habari zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni zinadai kwamba Lulu baada ya kuachiwa kwa dhamana ni kwenda kuzuru kaburi la marehemu Kanumba.
Inadaiwa kuwa, hilo litafanyika kwa sababu za kibinadamu zaidi kwa kuwa, marehemu na Lulu walikuwa watu waliofahamiana kikazi achilia mbali kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati yao.
Licha ya dhamana kuwa wazi, Lulu alirejeshwa gerezani mpaka jana ambapo taratibu za dhamana zilipokamilika.

No comments:

Post a Comment