FID Q ATUNUKIWA CHETI MAALUMU NA UNDER THE SAME SUN
Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Kubanda a.k.a
Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye
ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma Under The Same Sun kwa mchango wake
mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa
kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu
kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.
baada ya miezi kadhaa walirudi tena kanda ya ziwa
kuwarudishia shukurani wakaazi wa kanda ya ziwa kwa sababu mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi (albino) yalipungua sana hivyo kampeni yao kwa kushirikiana na
wakaazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa.
No comments:
Post a Comment