TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, January 13, 2013

MASTAA WANNE WAPIGWA STOP KUKANYAGA ARUSHA
KALAPINA:Kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga chenye maskani yake mitaa ya block 41 Jijini Dar.
Huyu amekuwa kwenye tageti ya masela hao kitambo kufuatia bifu lake na wanamuziki wa Nako 2 Nako ambapo miaka kadhaa ilioyopita mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo lenye umaarufu mkubwa Arusha alidaiwa kutekwa na kupigwa hadi kuvunjwa taya na wanamuziki wa Kikosi cha Mizinga hali iliyoleta uhasama hadi leo licha ya tukio hilo kutokuwa na ushahidi wa kutosha.

DIAMOND THE PLATINUM:Macharii hao walisema kuwa licha ya kosa lake sio kubwa sana lakini wanammaindi kutokana na mwaka jana kushindwa kufika kwenye onesho la muziki ambalo ilibidi atoe burudani.
Watu wengi walitoa kiingilio chao tena shilingi elfu kumi kumi matokeo yake hakufika ukumbini kwa madai ambayo baadae aliyatoa kwenye vyombo vya habari kuwa ndege ilimuacha. 
Waliongeza labda akitaka usalam aende akawaimbie shoo bure tena uwanjani na kuwaomba radhi watakuwa wameyamaliza.

BOB JUNIOR: Utozi ulimponza,Macharii hao walisema kuwa mwaka jana mwanamuziki huyo alienda kufanya shoo lakini macharii hao waliamua kumbadilikia kwa kumrushia makopo ya maji stejini pamoja na mayai hali iliyopelekea kuokolewa na mabaunsa pamoja na polisi,kisha wakamwambia asirudi tena Jijini humo


OMMY DIMPOZ:Yeye amejipalia mkaa kwenye sakata lake na Load Eyez  la kumtuhumu kuiba vifaa vya gari ya Ommy hali ililosabasha mwanamuziki huyo nyota wa kundi la Nako 2 Nako kwenda jela miezi kadhaa.
.
Hali hiyo ilionekana kuwa kera sana macharii hao na kusema wanamsubiri kwa hamu kubwa aende A Town wakamletee noma

No comments:

Post a Comment