TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, January 14, 2013

MAPOZI YA WEMA NA JB YAWAACHA HOI WAKAZI WA KONDOA
Wema na JB

Mtazamaji wa pozi hizo utajipa majibu kama wazee hao walikuwa sahihi kukerwa na kitendo hicho ama lah

Hapo endelea kujipa majibu Wema na JB
WAIGIZAJI  wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Jacob Steven ‘JB’ wamezua minong’ono baada ya kugandana kimahaba hadi wakawakera maustadhi.......
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari  lilijiri katika Kijiji Cha Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mastaa hao walikwenda kuzindua mpango wa Kilimo Kwanza, Ajira kwa Vijana ulioongozwa na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati.
Waigizaji hao walionekana kupeana ‘kampani’ kwa kila walichokifanya, huku kila mmoja akigandisha mkono kiunoni kwa mwenzake na kushikanashikana hadharani huku Wema akideka na kile kisauti chake kinachoweza kumtoa nyoka haraka pangoni.
Hawa wasanii wetu bwana, hebu waone wale (Wema na JB), muda wote wameshikana vile. Mh! Ndiyo nini sasa?” alisikika mmoja wa maustadhi aliyejitokeza katika uzinduzi huo.

Wakiwa mashambani, ulifika wakati wa mastaa hao kulima kwa kutumia trekta ambapo JB alionekana akimbeba Wema na kumsaidia kupanda kwenye trekta kisha akamsaidia tena kushuka baada ya kumaliza kazi.
Baada ya uzinduzi kufanyika mashambani na kila mmoja kutoa neno la kuhamasisha vijana kujiajiri kupitia kilimo, wasanii hao waliendelea kugandiana, jambo lililosababisha maustadhi kuendelea ‘kuwamaindi’ kabla ya kusoma dua na kuagana ambapo JB alimbeba Wema na kumpakiza kwenye gari lao aina ya Toyota Noah, wakaelekea kwenye gesti waliyofikia kijijini hapo tayari kwa kuendelea na ratiba nyingine.

Katika safari hiyo, mastaa hao waliambatana na wenzao wanaounda Bongo Movie Unity, Irene Uwoya, Single Mtambalike ‘Richie’ na Vincent Kigosi ‘Ray’

No comments:

Post a Comment