TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, January 13, 2013

BABY J AFUNGUKA KUHUSU UJIO WAKE WA NGOMA MPYA






















MSANII wa kike anayefanya poa kwenye game kutoka pande za Zenji Baby J, amefanya mahojiano maalumu na mwandishi wa makala hii  na kusema kuwa ndani ya mwaka huu amejipanga kikamilifu ikiwa pamoja na ujio wa mzingo wake mpya anaomalizia kufanya na msanii Diamond unaokwenda kwa jina la ‘Nimempenda Mwenyewe’.

Baby J alisema kuwa ujio wa ngoma hiyo utakuwa wa kipekee kwani amejipanga kwa lengo la kufanya kazi kwa sababu tayari amekua kiakili, mawazo na hata kimuziki baada ya kufanya kazi kibao ndani ya mwaka uliopita ambazo zimempa nafasi kubwa ya kujiamini zaidi.

Alisema kuwa sambamba na ujio wa ngoma hiyo pia suala la wasanii wengi kutoka Zanzibar na kuja kufanya muziki Tanzania Bara linatokana na aina ya muziki ambao umekuwa ukifanywa visiwani humo ambao ni taarabu na hivyo miziki ya kisasa inaonekana ya kihuni kutokana na maandali yaliyomo visiwani humo.
 
Alisema kuwa sambamba na maandili pia Zanzibar ni ndogo hivyo wanalazimika kuja DSM, ingawa kwa upande mwingine wamekuwa wakipokelewa vizuri na mashabiki wa Zanzibar kutokana uwakilishi wao.

“Naweza kusema Zanzibar muziki ambao umekuwa ukijulikana zaidi ni taarabu na mingine ya asili hivyo aina ya mizki yetu sisi haipewi nafasi sana kutokana na maadili kwani muziki wetu unaonekana unavunja baadhi ya maadili lakini hata hivyo si kwamba hauna soko bado unapokelewa vizuri,” alisema.

Baby J alizungumzia suala la kutotoa albamu ambapo alisema kuwa kwa upande wake hawezi kuachia albamu ingawa ana ngoma nyingi ambazo zinaweza kufika hata albamu mbili, lakini anaona ni vizuri kutoa single kwani ndizo zinazolipa vizuri kwa sasa.

Juu ya kufanya kazi za nje alisema kuwa ana mipango ya kufanya ngoma na msanii wa Kenya Amani, alidai ni nyota ambaye amekuwa akimkubali toka kitambo, hivyo  ndani ya mwaka huu atakuwa amefanya naye kazi ingawa wapo pia wasanii wengine wa nje ya Tanzania anaotarajia kushirikiana nao.


Kwa upande wa maisha binafsi Baby J ameweka wazi kuwa tayari ameshaolewa na sasa yupo kwenye ndoa ambapo alifunga pingu za maisha Aprili mwaka jana, lakini mume wake anaishi nchini Marekani ambapo kwa mipango aliyonayo naye anaweza kwenda kuishi huko baadae.


“Nimeshaolewa ingawa ndoa yetu ilikuwa ni siri lakini ndo hivyo na sikutaka watu wajue juu ya hilo, ingawa namshukuru Mungu kwa sasa nipo kwenye ndoa maisha yanaenda vizuri tu,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment