SAJENT SIJAWAHI KUTOKA NA RAY KIMAPENZI
BAADA ya ishu kuvuja kuwa msanii wa filamu Husna Idd ‘Sajenti’,
ana mahusiano ya kimapenzi na ’Ray’, amezikana habari hizo huku
akisisitiza kuwa msanii huyo anamchukulia kama kaka yake na suala la
kutoka naye kimapenzi halina ukweli wowote.
Tukio la Sajenti kutoka na Ray lilianza kuskika pindi kundi la bongo movie lilipoenda mkoani Mwanza kucheza mchezo wa kirafiki na wasanii wa mkoani humo.
Mtandao huo ulitaka kujua Sajenti anazungumziaje habari hizo, ambapo alidai kuwa hajawahi kutoka na ’Ray’ kimapenzi na anayesambaza ishu hizo ana nia ya kumchafua ingawa alishindwa kueleza anachafuliwa kwa namna gani.
Alisema kuwa kama zingekuwa na ukweli taarifa hizo angeweka wazi lakini haoni sababu ya kukubali wakati kitu hajawahi kukifanya na wala hana wazo wa kutoka na msanii huyo kwani mpenzi wake anamtosha.
“Sijawahi kutoka kimapenzi na Ray na hajui hata nguo yangu ya ndani na kama una ukweli kama unajua natoka naye kwanini umepiga simu na kuniuliza,??.. nasema sijawahi kutoka naye,” alidai.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kama mwanaume aliwahi kutoka naye hawezi kuficha lakini juu ya Ray atakanusha siku zote.

No comments:
Post a Comment