TAARIFA ZAIDI KUHUSU EMANUEL OKWI
Mwandishi wa habari za michezo
Shaffih Dauda ameripoti kwamba ile ishu ya mchezaji wa kimataifa wa
Uganda anayeichezea klabu bingwa ya Tanzania Bara Simba SC, Emmanuel
Okwi kwenda kujiunga na kambi ya Simba iliyopo nchini Oman imefikia
mwisho.
Taarifa za ndani kutoka Simba
ni kwamba timu hiyo imefikia maamuzi ya kumuuza mshambuliaji huyo kwenda
Etoile du Sahel ya Tunisia kwa ada ya uhamisho itakayovunja rekodi ya
uhamisho hapa nchini ya dola za kimarekani laki tatu.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya
Simba Mh. Aden Rage kwa sasa yupo nchini Tunisia akisimamia taratibu
zote za uuzwaji wa Okwi ambaye alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Simba
hivi karibuni.
“Ni kweli Mwenyekiti yupo
Tunisia akishughulikia uuzwaji wa Okwi kwa klabu ya Etoile du Sahel, ada
ya uhamisho ni dola laki tatu na muda mchache ujao dili litakamilika na
Okwi atapewa ruhusa ya kuzungumza maslahi binafsi na klabu yake mpya.” –
kilisema chanzo cha habari kutoka Simba.
Etoile du Sahel ni klabu
mojawapo yenye mafanikio makubwa barani Afrika ikiwa inashikilia rekodi
ya kuwa klabu pekee barani afrika kushinda kila kombe linaloandaliwa na
CAF, shaffih anapatikana kwenye shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment