SIJUTII KUKOSA TUZO ZA KORA NA BADALA YAKE NAJIVUNIA MAMBO MENGI NILIYOJIFUNZA- DOGO ASLAY
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Aslay Sadiq 'Dogo Aslay' amefunguka aliyoyakuta nchini Ivory Coast alipoenda kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kora
Msanii huyo ameeleza kuwa amejifunza mengi kutokana na safari yake hiyo.Moja kubwa ni wasanii kujiheshimu ili kuongeza uwezo wa kazi zao na kuwa wa kimataifa
Alifunguka hayo msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Aslay Sadiq 'Dogo Aslay' baada ya kurudi nchini akiwa ametoka nchini Ivory Coast kwa ajili ya kinyaga'nyiro cha tuzo za Kora ambapo hakufanikiwa kurudi na tuzo.
Alisema kuwa heshima ndio kitu kikubwa cha msingi ili uweze kuendelea katika kazi ya sanaa na kuweza kuzidi kukubalika kwa kila kazi ufanyayo.
"Nimewaona mastaa wengi ingawa wengine sijui wametokea nchi gani na ni wa kina nani ila kikubwa nilichokiona kwao ni heshima walio nayo, hiyo ni tofauti kubwa kati ya wasanii wa nje na sisi hapa hivyo tunatakiwa tubadilike" alisema Aslay.
Aliongezea kuwa mbali na hayo amejifunza jinsi ya kuishi na watu wa aina mbalimbali na kujua wenzao wanafanya nini katika sekta ya sanaa kiujumla.
Pamoja na hayo Aslay alisema kuwa kukosa tuzo hiyo kwake ni kama changamoto, na anajipanga kufanya kazi nzuri ili ziweze kukubalika.
Dogo Aslay alikwenda nchini Ivory Coast kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kora ambapo yeye aliingia katika kipengele cha msanii bora chipukizi lakini hakufanikiwa kupata tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment