WANACHUO WACHAMBUA SERA MBOVU ZA SERIKALI UN
Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw.
Amani Ngusaro akitaja baadhi ya vikwazo vinavyo kwamisha uboreshaji wa
Mazingira katika maeneo ya makazi ikiwemo uhaba wa maji na kutaka
vikwazo hivyo viangaliwe upya na kuboreshwa sambamba na kutolewa kwa
elimu ya Mazingira na uhamasishaji katika ngazi
zote
Wanafunzi
kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini wakitoa maoni yao katika mjadala wa
wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo wamelalamikia baadhi
ya Sera za Serikali zisizotekelezeka wakati wa maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67.Aidha Afisa Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika alitoa nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na mazingira. Aidha pia ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa sio jambo la mzaha hivyo serikali inatakiwa kuwa na sera madhubuti zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga hilo ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika hali bora
No comments:
Post a Comment