MKUTANO WA MAJAJI NA MABALOZI WAANZA JIJINI ARUSHA
Pichani
ni Waziri wa sheria na katiba Mathias Chikawe akiwa na Jaji wa mahakama
ya Afrika ya haki za binadamu kwenye ufunguzi wa mkutano wa shughuli za
mahakama uliowashirikisha mabalozi kutoka nchi za umoja wa Afrika (AU) unaondelea kwenye ukumbi wa hotel ya Mount Meru jijini hapa(picha na
mahmoud ahmad Arusha)
RAIS
wa mahakama ya Afrika( Africa court) kutoka nchini Ghana Sophia
Akuffo amefungua mkutano wa kamati ya kudumu ya umoja wa
Afrika(AU) uliokutanisha majaji pamoja na mabalozi 54 kutoka nchi za Umoja wa Afrika ulionza leo
Akifungua mkutono huo Raisi wa mahakama ya Afrika Sophia Akuffo
amezitaka nchi za bara la Afrika kuweka muda na kutekeleza kwa vitendo
na kuifahamisha jamii ya waafrika juu ya haki za binadamu na viongozi
kuacha kukiuka haki hizo
.
Alisema kuwa katika mkutano huo washiriki wataweza kuangalia kwa
undani mahusiano yaliyopo kati ya mahakama ya kutetea haki za binadamu
pamoja na kamati ya wawakilishi ya umoja wa mataifa katika kuhakikisha
kuwa mahakama za Afrika zinaboreshwa.
Aidha alisema kuwa mkutano huo utaweza pia kuunganisha ushirikiano
kati ya mahakama na mashirika mengine ya umoja wa afrika pamoja na
kamati ya kudumu ya wawakilishi wa umoja huo ili kuhakikisha kuwa
wanafanikiwa katika mambo mbali mbali .
“mkutano huu ni muhimu sana kwani majaji na mbalozi wataweza
kujadili mambo mazuri ambayo yayawezesha hata mahakama kuondokana na
baadhi ya changamoto zinazowakabili”alisema Uwanone
Aliongeza kuwa katika mkutano huo wataweza kuweka mkakati juu ya
Mahakama na kuweza kubuni njia mbali mbali ambazo zitaweza kulinda
haki za binadamu ndani ya afrika.
Alieleza kuwa kamati ya wawakilishi ya kudumu ya umoja wa mataifa
itaweza kuweka umakini mkubwa kwenye mahakama za Afrka kwa kuwa hiyo
ni moja ya sera zilizoko ndani ya umoja wa mataifa.
Hata hivyo mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbali mbali wa mahakama
ya haki za binadamu akiwemo makamu wa rais wa mahakama hiyo
,mwenyekiti wa kamati ya wawakilishi wa umoja wa mataifa pamoja na
muwakilishi wa kamati hiyo.
No comments:
Post a Comment