![]()  | 
| Wananchi wa Rukwa wakiwa wanatoa maoni yao juu ya uundwaji wa Katiba Mpya. | 
Wananchi wa sumbawanga leo wamepata 
nafasi ya kutoa maoni kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya,mbele ya 
wajumbe wa tume ya katiba, wananchi wamepata fursa ya kuchangia yale 
wanayodhani yanafaa kuwemo katika katibu mpya.
Wapo waliochangia kwa kuongea pia wapo waliochangia kwa njia ya maandishi 
Jambo Kubwa  ambalo limejitokeza katika 
mchakati huo ni suala la dini wengi watoa maoni wamekuwa wakizungumzia 
suala la dini , mfano mtu mmoja alisema angependa kwenye katiba 
ingeonyesha kuwa siku ya kuabudu waislamu ijumaa kuwa ni  siku ya 
mapumziko kama ilivyo siku ya jumapili kwa wakristo.
Kama hiyo haitoshi nimeweza kuzungukia baadhi ya vijiwe vilivyo katikati ya mji wa sumbawanga ikiwa ni pamoja na soko la mitumba lililo jirani na uwanja wa kumbukumbu ya Nelson Mandela jirani na njia ya kwenda mkoa wa katavi nako huko hoja inayotawala ni suala la dini.
Je mwananchi mtanzania mzalendo unaona mchakato huu ukiegemea kwenye hoja ya dini na si mambo mengine tutapata katiba tunayoitataka?.
Mkami Jr
Mjengwa Blog -Sumbawanga 

No comments:
Post a Comment