TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, October 27, 2012

MTOTO WA KIBRAZIL ASIYEKUWA NA MAKANYAGIO ATIMIZA NDOTO YAKE YA KUKUTANA NA MESSI.
Mtoto Gabriel akicheza mpira na nyota wake Lionel Messi wakati alipopata mwaliko wa kutembelea kambi ya Barcelona

Gabriel akipiga danadana mbele ya shujaa wake Messi ambaye hayupo pichani kumdhihirishia kuwa naweza kufanya vitu vikubwa japo sina makanyagio

Lionel Messi akisaini jezi ya mtoto huyo kwa furaha baada ya kushangazwa na kipaji chake cha uchezaji wa mpira

Wachezaji wa Barcelona wakipiga picha na Gabriel kutoka kushoto ni Victor Valdes,Beki Adrioan na Dani Alves























GABRIEL Muniz ni mtoto wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 11 ambaye alikuwa na ndoto za kukutana na Lionel Messi siku moja. Na ndoto yake hatimaye imetimia, hasa baada ya habari yake kuwa maarufu na kuwagusa wengi mioyoni huku pia ikiwapa changamoto ya kutokata tamaa ya maisha.

Gabriel hana makanyagio. Alizaliwa hivyo hivyo. Ingawa familia yake ilidhani kwamba angekuwa na matatizo makubwa katika maisha yake ya kawaida, alianza kutembea kabla hajatimiza umri wa mwaka mmoja. Ilimchukua muda mrefu kuweza kuruka kutoka kutembea hadi kucheza mpira, lakini aliweza yote hayo. Na, hakika, hakuna anachopenda zaidi ya kucheza soka.

Anacheza bila ya viatu, na hutumia vifaa maalum kuvaa chini inaponyesha mvua ili kumuepushia kuteleza. Ukimuangalia anavyocheza mpira utashangaa. Ana kasi na "maujuzi" – anaki paji sana na anafanya kila awezalo kumuiga shujaa wake, Leo Messi.

Gabriel alikuwa na bahati sana kualikwa katika wakati wa mazoezi ya Barcelona, na mwishoni mwa mazoezi akapata fursa ya kukutana na wachezaji, na kuzungumza nao hasa Wabrazil wenzake Dani Alves na Adriano.

Lakini tukio lake kubwa zaidi lilikuwa halijawadia. Pale kocha Tito Vilanova alipomuuliza kama amepata fursa ya kukutana na wachezaji wote, Gabriel alijibu: "Sijaonana na Messi bado".

Hatimaye 'mchawi' huyo wa Kiargentina akatokea. Wote wakaanza kuuchezwea mpira na Messi akapigwa na butwaa pale alipoona ufundi wa kuchezea mpira alionao Mbrazil huyo mdogo.

Ilionekana kama ni jambo lisilowezekana kwa mtoto asiye na makanyagio kukimbia na kukokota mpira, achilia mbali kupiga 'vibaiskeli', matobo na tikitaka, lakini yeye anaweza.

No comments:

Post a Comment