SIMU ZA KICHINA ZOTE ZAPIGWA MARUFUKU NCHINI KENYA
Stori
kubwa Kenya ambayo hata kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM october 1, 2012
imeshika nafasi ya kwanza ni kuhusu mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya
kuzizima kiteknolojia simu zote zilizofeki ambazo zimekua zikitumiwa na
wakenya.
Mtangazaji
wa Citizen Tv/Radio William Tuva ameripoti kwamba wakenya walionunua
simu feki wapo kwenye wakati mgumu na itawabidi wanunue simu original
kwa sasa ili kurudi tena kwenye mawasiliano.
Ameripoti
pia kwamba inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa Safaricom
peke yake ni wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao kuzimwa kwa
sababu ni feki.
Kwenye
line nyingine Tuva ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni ya
shilingi kutokana na simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa njia
ambayo sio halali.
Baadhi
ya wananchi ambao simu zao zimefungwa wamekaririwa wakisema waliamka
asubuhi na kukuta simu zao hazifanyi kazi, kumbe tayari zimeshazimwa
kiteknolojia na tume ya mawasiliano nchini humo ambapo kwa mujibu wa BBC
na wateja milioni mbili na nusu ambao simu zao zimezimwa.
Mmoja
wa watu hao amekaririwa akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa 11
niamke, sikusikia naamka tu naona nje kunapambazuka na simu yangu
wamezima’
No comments:
Post a Comment