MKATABA WA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO WASAINIWA
 Mtendaji Mkuu wa Tan roads Mhandisi Patrick 
Mfugale (kushoto) na  Mtendaji Mkuu kutoka kampuni ya ujenzi ya China 
Railway 15 Bureau group Corporation (CR15G) Zhang Tonggang 
(kulia) wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa daraja la  Kilombero lenye 
urefu wa  meta 384 na ujenzi wa barabara zake za miingilio za lami( 
kilometa 9.142)  zoezi hilo litagharimu shilingi bilioni 53.2 
Hafla hiyo imefanyika Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Dkt, John Magufuli ,katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Herbert Mrango Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Tanroads Bi. Hawa Mmanga , Mbunge wa Mikumi Abdul Salim Ameir na Mbunge kutoka Morogoro Kusini Innocent Kalgeris .
Ujenzi wa daraja hilo 
utaziunganisha Wilaya za Mahenge na Ulanga pamoja na kuboresha Usafiri 
wa mikoa ya kusini  na kuleta kichocheo cha ukuaji wa shughuli za 
kiuchumi. (Picha na Mwanakombo Jumaa-Maelezo)  
 
No comments:
Post a Comment