WAISLAM DAR WACHACHAMAA KWA KUKAMATWA SHEIKH PONDA
Kamanda
 wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova akitoa 
taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya 
na Taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ambapo amefafanua
 kuwa pamoja na mambo mengine Sheikh huyo anahusishwa na kundi 
lililovaamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika 
Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA.
Jeshi
 la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa 
Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
Akitoa
 taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya 
Polisi ya Dar es Salaam Sulemain Kova amesema amesema jeshi hilo 
limechukua hatua hiyo kutokana na Sheikh huyo kutuhumiwa na makosa 
mbalimbali ya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.
Hata
 hivyo leo katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa na patashika katika ya 
polisi wa kutuliza ghasia baina ya waandamanaji waliokuwa wakitaka 
Sheikh huyo kuachiwa pamoja waumini wengine wanashikiliwa.

No comments:
Post a Comment