TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, October 5, 2012

MAHABUSU WAPORA ASKARI POLISI BUNDUKI NA KUTOROKA

Mahabusu wawili wanodaiwa kuwa na kesi ya mauaji wametoroka wakiwa chini ya ulinzi wa polisi katika Mahakama Kuu jijini Arusha baada ya kumkaba askari aliyekuwa anawalinda kisha kumpokonya bunduki aina ya SMG na kukimbia nayo
Habari zilizopatikana toka kwa mashuhuda wa tukio hilo na kudhibitishwa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas baada ya mahabusu hao kufanikiwa kumpora askali silaha hiyo, waliruka uzio na kuingia katika mto uliokuwa karibu na mahakama na kutokomea kusikojulikana.
Hata hivyo polisi waliingia msako wa kuwasaka mahabusu hao na kufanikiwa kuikuta silaha ikiwa imetelekezwa juu ua jiwe katika mto huo ikiwa na risasi zote.
Aidha mahabusu hao walipata upenyo wa kutoroka baada ya kutoka katika chumba cha mahabusu na kuelekea kupanda karandika ili warudishwe gereza za la Kisongo walipokuwa wamehifadhiwa.

No comments:

Post a Comment