ALEX FERGUSON NA RIO WAMALIZA MZOZO
Kocha wa Manchester United Sir 
Alex Ferguson amesema ameshayamaliza na mchezaji wake Rio Ferdinand 
ambae weekend iliyopita kwenye game na Stoke City aligoma kuvaa t-shirt 
ya kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi kwenye soka ambapo ndio alikua 
mchezaji pekee ambae hakuvaa t shirt ya hiyo kampeni.
Fergie amesema aliaibika 
kutokana na hicho kitendo cha Rio lakini baadae aligundua ilitokana na 
tatizo la mawasiliano ila kwa sasa tayari ameshafanya nae mazungumzo 
hivyo sio ishu kubwa tena manake wameyamaliza ambapo Fergie amesema pia 
kwamba Rio ataongezewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya huu wa sasa 
kuisha.
Ukiachia Rio Ferdinand ambae 
mdogo wake Anthony Ferdinand wa QPR alikua na ishu ya ubaguzi kutoka kwa
 John Terry hivi juzi, zaidi ya wachezaji 30 kwenye Premier League 
wamepinga hiyo kampeni.

No comments:
Post a Comment