CHRISTIANO RONALDO ATAKA KUWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KULIPWA KIASI CHA £400,000 KWA WIKI

 
Mchezaji wa Real Madrid Cristiano 
Ronaldo anataka kuwa mcheza soka wa kwanza kupokea mshahara wa £400,000 
kwa wiki, kwa mujibu chanzo cha habari cha ESPN.
Kutokana na sheria za kodi za Spain  
zilivyo, Ronaldo atahitaji kufikia kulipwa mshahara wa £400,000 kwa wiki
 ili kuweza kupata anachokitaka kuwa mchezaji anayepokea fedha nyingi za
 mshahara.
Huku akiwa anavivutia vilabu vingi 
dunaiani, wakiwemo matajiri wa Man City na PSG, mazungumzo ya juu ya 
hatma ya Ronaldo yapo njiani kuanza.
Ronaldo ametoa taarifa rasmi akisema 
kwamba 'huzuni' yake aliyosema anayo haihusiani na mambo ya fedha. 
Lakini chanzo cha habari kilicho karibu na Ronaldo kinasema kwamba Mreno
 huyo anataka mshahara wake uongezwe mara mbili, na hili litafanya 
aamini kwamba klabu hiyo ipo tayari kumpigania aendeleee kubaki kwenye 
klabu hiyo.
Nahodha huyo wa Ureno aliwahi kuwa 
mchezaji anayelipwa vizuri zaidi duniani wakati akihamia Mafrid mwakak 
2009, akiwa analipwa £200,000 kwa wiki, lakini kwa sasa amejikuta 
ameteremka mpaka kushika nafasi ya kumi duniani, akipitwa na wachezaji 
kama Samuel Eto'o, Wayne Rooney, Neymar na Didier Drogba pamoja na 
wengine watano.
Kingine, Madrid kwa sasa wanamiliki 
asilimia 50 ya haki za picha za Ronaldo, na sasa tayari ameshampita 
David Beckham kuwa mchezaji ambaye jezi zake zinauzwa sana katika 
ulimwengu wa soka.
Ronaldo ana mkataba na Madrid unaoishia 2015.
 
No comments:
Post a Comment