TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 10, 2012

CRISTIOANO RONALDO ANUNUA GARI MPYA LENYE THAMANI YA SH.MILLION 415. JAMAA ANATISHA KWA KUTEMBELEA MAGARI MAKALI
























ADRID, Hispania
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejawa na furaha tele kutokana na kiwango cha juu alichoanza nacho msimu huu na kuamua kujipongeza kwa kujinunulia gari dogo jipya la kifahari kwa ajili ya kutanulia mitaani.

Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh. milioni 415).

Sifa mojawapo kubwa ya gari hilo la kisasa ni kasi yake ya kuchanganya mwendo kwani linapowashwa tu, huwa na uwezo wa kufikia spidi ya kilomita 100 kwa saa baada ya muda mfupi wa sekunde 3.1.

Ronaldo alionekana juzi katika maeneo ya kwao, Lisbon nchini Ureno ambako amekwenda kuungana na wenzake katika kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.  

Mbali na gari hilo jipya (McLaren MP4-12C Spyder) Ronaldo pia anamiliki magari kadhaa ya kifahari likiwamo aina ya Lamborghini Aventador LP700-4.

No comments:

Post a Comment