TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, October 18, 2012

"HUWEZI KUNIPATA BILA YA KUWA NA MILLION MOJA - JACK WOLPER"



WAKATI filamu nyingi za bongo bajeti yake si ile ya kushtua mtu kama kazi za wasanii wa mbele, na kwa kulitazama hilo msanii Jackline Wolper ameamua kuweka wazi fungu lake ili kwa wale wanaotaka kumshirikisha kwenye filamu zao basi wajue kuwa anaweza kucheza kuanzia milioni 1 na kuendelea chini ya hapo hapotezi muda.

Wasanii wa Tanzania wanatatizo kubwa la kutotumia pesa ya kutosha katika utengenezaji wa filamu zao, na wengi bajeti zao ni chini ya mil 8, hivyo kwa kiasi anachokitaka Wolper sijui kama ni kweli anaweza kulipwa ingawa wengi tumewazoea wakisema hivyo lakini mwisho wa siku unasikia kacheza filamu kwa laki 2.


Msanii huyo aliweka wazi ishu hiyo wakati akizungumza kwenye mahojiano na televisheni ya Clouds TV kupitia kipindi cha Take One, ambapo aliulizwa kiasi anachotaka kulipwa kucheza filamu, ndipo alipotaja fungu hilo.

No comments:

Post a Comment