MAJINA YA WALIOHUSIKA KUMUUA KAMANDA BARLOW YATAJWA
wandishi wa habari Albert G Sengo kutoka Mwanza ameripoti kwamba majina ya watu watano wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Leberatus Barlow yametajwa na Polisi.
Akitaja hayo majina mbele ya 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa upelelezi 
wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba  amesema simu iliyoporwa ya 
mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo 
imesaidia kukamilisha upelelezi huo na wahusika kukamatwa. 
Waliotajwa kuhusika na hayo 
mauaji ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye 
aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48), 
 Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote 
wamekatwa wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.
lisema Kikosi kazi cha 
upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi 
matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na jingine la intelijensia 
huku wakitumia njia ya sanyansi kufatilia kupitia mitandao ya simu.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao 
wa Dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi 
linasaka wengine  Lakini chanzo cha hao wauaji kufanya hivyo bado 
hakijatajwa.
Liberatus Barlow aliuawa Oktoba
 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana 
katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita 
kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao 
cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji. 

No comments:
Post a Comment