DK. BILAL KUFUNGUA MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WANAWAKE
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema kuwa mkutano huo ambao ni wa saba (7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za Afrika Mashariki.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.
Amesema kuwa mkutano huo utakuwa fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi ya kuwainua kiuchumi akinamama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara Wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi akinamama.
Aidha, Riyami amesema kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es Salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanyabiashara wanawake kwa nia ya kuimarisha umoja wao.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo amewasisitiza wajumbe wa mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo saa 1.30 Asubuhi. Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00
No comments:
Post a Comment