TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 24, 2012

TAARIFA KAMILI KUHUSU BOBAN NA NYOSSO KUSIMAMISHWA KUCHEZA SIMBA























Club ya Simba imeleza kuhusu kuwasimamisha wachezaji wake wawili ambapo wa kwanza ni Haruna Moshi Shaaban (Boban aliesimamishwa kuichezea timu ya wakubwa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu na kutokuwa na heshima kwa mwajiri (timu) ambapo klabu imempa muda wa siku 21 kutoa maelezo kuhusu makosa yake lakini akishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, klabu inaweza kumchukulia hatua zaidi.
Katika kipindi hicho (siku 21 kuanzia jana), Boban atapokea nusu ya mshahara wake wa kila mwezi na hatopata marupurupu yoyote yanayohusiana na timu ya wakubwa
Kwa upande wa Nyoso, uongozi umemwagiza afanye mazoezi na kikosi cha timu ya pili (Simba B) hadi atakapoimarisha kiwango chake cha uchezaji, hii imetokana na ripoti ya benchi la ufundi iliyoonyesha kwamba mchezaji huyo amekuwa akifanya makosa mengi ya kiuchezaji yanayoigharimu klabu yake japo amekuwa akipewa maelekezo na walimu lakini bado amekuwa akirudia makosa yaleyale.
Kutokana na hilo, Nyoso atafanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha pili hadi walimu watakaporidhika kwamba amejirekebisha na yuko tayari kutumikia kikosi cha wakubwa ambapo kwa muda wake wote huo akifanya mazoezi na timu B, Nyoso atakuwa akipata mshahara wake wa kila mwezi kama kawaida na pia atapata marupurupu wanayopata wachezaji wa Simba B.

No comments:

Post a Comment