RICK ROSS KUTUMBUIZA JUKWAA LA FIESTA OCTOBER 06,2012
Msanii
nyota kutoka nchini Marekani, mzaliwa wa nchini Marekani,
anayetambulika kwa jina la kisanii kama Rick Ross, ambaye kwa jina
halisi anajulikana kama William Leonard Roberts II, anatarajia kutua
nchini Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kushiriki kikamilifu
kushambulia jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, litakalofanyika Oktoba 6
ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika
kuhakikisha mambo yanakwenda sawa bin sawia kwa kila idara kuhusiana na
tamasha hilo, waandaaji ambao ni Prime Time Promotions Ltd
wakishirikiana na Clouds Media Group huku mdhamini wao mkubwa ikiwa ni
kampuni ya bia ya Serengeti,wameandaa shamara shamra mbalimbali za
kuhakikisha tamasha hilo mpaka linafika kileleni,linaamsha na kuacha
gumzo la kipekee kabisa miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji
vyake, ikibidi mpaka Kigoma mwisho wa reli kwa namna moja ama nyingine.
Msanii huyo mwenye umahiri mkubwa wa kufloo awapo jukwaani mpaka sasa anatamba na nyimbo/albamu kadhaa kama vile Hold Me Back 2012 God Forgives, I Don't, Hustlin' 2006 Port of Miami Diced Pineapples 2012 God Forgives, I Don't So Sophisticated 2012 God Forgives, I Don't 911 2012 God Forgives, I Don't Stay Schemin 2012 Rich Forever Aston Martin Music.
Nyinginezo ni 2010 Teflon Don DJ Khaled 2008 Trilla Lemme See 2012 So Sophisticated Amsterdam 2012 God Forgives, I Don't Black Magic 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire The Boss 2008 Trilla You the Boss 2011 You the Boss Touch'n You 2012 Touch'N You Bag of Money 2012 Maybach Music Group Presents Self Made, Vol. 2: The Untouchable Empire.
No comments:
Post a Comment