SAKATA LA DAWA FEKI ZA ARV TAARIFA ZAIDI ZATOLEWA
Waziri wa Afya Dk. Hussein Mwinyi |
Kiwanda cha kutengeneza dawa
cha Tanzania Pharmacetical Industrial (TPI) kimesema Serikali inabidi
iharakishe uchunguzi kuhusu mtu aliyeingiza nchini dawa bandia ya
kupunguza makali ya virusi vya ukimwi iitwayo TT-VR 30 ili kuondoa
wasiwasi ulioenea kwa watumiaji.
Mkurugenzi mtendaji wa TPI
Ramadhani Madabida amesema uchunguzi wa awali unaonyesha serikali
inamfahamu mtu alieingiza hizo dawa Tanzania, zilipotoka na tarehe ya
kuingizw hivyo kuharakishwa kwa mchakato huo kutakomesha mizengwe ya
baadhi ya wawekezaji kutoka nje kutaka kuchafua ubora wa bidhaa
zinazotengenezwa Tanzania.
Tayari serikali imewasimamisha
kazi Mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa nchini MSD Joseph Mgaya pamoja na
mkuu wa kitengo cha udhibiti ubora na afisa udhibiti ubora wa MSD
kutokana na kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo bandia ya kupunguza makali
ya virusi vya ukimwi.
No comments:
Post a Comment