MAGUFULI ATETA NA MAKANDARASI
  | 
| WAziri wa Miundo Mbinu John Magufuli azungumza na uongozi wa Kampuni ya Chico | 
  | 
WIZARA
 ya Ujenzi imewakumbusha Wakandarasi nchini kujenga barabara 
zinazolingana na thamani ya fedha, iliyopo kwenye mikataba yao. 
 
Agizo
 hilo limetolewa leo mkoani Singida na Waziri John Magufuli, wakati 
anakagua marudio ya ujenzi wa barabara, eneo la mlima Sekenke-Shelui, 
yenye urefu wa kilomita 33.3. 
 
Amesema
 serikali imetumia zaidi ya Sh.Bilioni 35, kugharamia ujenzi huo, lakini
 mkandarasi China Henan International Cooparation Group Co Ltd(CHICO), 
ilijenga chini ya kiwango. 
 
Aidha ameuagiza 
uongozi wa kampuni hiyo kuwapatia wafanyakazi wake vifaa vya kufanyia 
kazi, hasa viatu na gloves kwa ajili ya kuvaa mikononi.
 
Hata
 hivyo meneja TANROADS Mkoa Singida, Yustak Kangole amesema barabara 
hiyo baada ya kukamilika Januari, 2008, ilichukua miezi miwili kuanza 
kubomoka, kutokana na ujenzi hafifu.  
 
Kwa
 mujibu wa meneja mradi wa barabara hiyo, mhandisi Stone Chen, marudio 
ya ujenzi yanaigharimu kampuni zaidi ya S h.Bilioni kumi.  
Na Elisante John  
 
 | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
  | 
 
No comments:
Post a Comment