TAARIFA KAMILI KUHUSU BOBAN NA NYOSSO KUSIMAMISHWA KUCHEZA SIMBA
Club ya Simba imeleza kuhusu
kuwasimamisha wachezaji wake wawili ambapo wa kwanza ni Haruna Moshi
Shaaban (Boban aliesimamishwa kuichezea timu ya wakubwa kutokana na
vitendo vya utovu wa nidhamu na kutokuwa na heshima kwa mwajiri (timu)
ambapo klabu imempa muda wa siku 21 kutoa maelezo kuhusu makosa yake
lakini akishindwa kutoa maelezo ya kuridhisha, klabu inaweza kumchukulia
hatua zaidi.
Katika kipindi hicho (siku 21
kuanzia jana), Boban atapokea nusu ya mshahara wake wa kila mwezi na
hatopata marupurupu yoyote yanayohusiana na timu ya wakubwa
Kwa upande wa Nyoso, uongozi
umemwagiza afanye mazoezi na kikosi cha timu ya pili (Simba B) hadi
atakapoimarisha kiwango chake cha uchezaji, hii imetokana na ripoti ya
benchi la ufundi iliyoonyesha kwamba mchezaji huyo amekuwa akifanya
makosa mengi ya kiuchezaji yanayoigharimu klabu yake japo amekuwa
akipewa maelekezo na walimu lakini bado amekuwa akirudia makosa
yaleyale.
Kutokana na hilo, Nyoso atafanya mazoezi na
wachezaji wa kikosi cha pili hadi walimu watakaporidhika kwamba
amejirekebisha na yuko tayari kutumikia kikosi cha wakubwa ambapo kwa
muda wake wote huo akifanya mazoezi na timu B, Nyoso atakuwa akipata
mshahara wake wa kila mwezi kama kawaida na pia atapata marupurupu
wanayopata wachezaji wa Simba B.