TAZARA YAANDAA SAFARI YA SELOUS SIKU YA WAPENDANAO
UONGOZI wa
Shirika ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) umesema unaandaa safari
ya kitalii katika Hifadhi ya Selous maalum kwa Siku ya Wapendanao
‘Valentino’ itayofanyika Februari 14 kila mwaka.
Sababu hasa za kufanya hivyo ni
kutokana na mafanikio iliyopata katika safari iliyofanyika Desemba 29
mwaka jana katika kukamilisha sherehe za Sikukuu za mwisho wa mwaka.
Katika safari iliyopita iliyojumuisha wafanyakazi wa kampuni moja ya habari ilipokewa vizuri na watu wengi ambao waliwashukuru viongozi wa Tazara kwa kuwapa nafasi hiyo licha ya kuwa walichelewa kutoa taarifa ya kuwepo kwa safari hiyo.

Akizungumzia mrejesho wa safari
iliyopita, Meneja Masoko wa Tazara Hemed Msangi alisema ziara hiyo
ilikuwa na mafanikio makubwa kwa sababu watu wengi waliitikia vizuri
tofauti na matarajio yao.
Sababu hiyo inawafanya kuandaa safari nyingine tena ili kuwaridhisha wateja wao.
Sababu hiyo inawafanya kuandaa safari nyingine tena ili kuwaridhisha wateja wao.
“Tumepanga kuwapeleka tena wateja wetu
katika Hifadhi ya Selous tarehe 16 Februari mwaka huu ili kutoa nafasi
ya kufurahi pamoja katika Siku ya Wapendanao ambayo hufanyika Februari
14 kila mwaka, hivyo wananchi wajiandae tena,” alisema Msangi.
Msangi aliongeza kuwa kwa sasa
wanawasiliana na wadau wengine ili kukamilisha maandalizi ya safari hiyo
ili iwe na mafanikio makubwa zaidi ya ile iliyofanyika mwishoni mwa
mwaka jana.
“Tumepata changamoto nyingi katika
safari iliyopita, vilevile tumepata maoni mengi ya namna ya kuboresha
huduma yetu hivyo tunaahidi kuwa tutayafanyia kazi maoni yote
yaliyotolewa na kuhakikisha kuwa tunakidhi haja za wateja wetu,” alisema
Msangi.
No comments:
Post a Comment